Description of image Joining Instruction 2025-2026   |   Description of image Financial Statement for the Year Ended June 2023
Register now
Top level banner

BENKI KUU YA DUNIA YATEMBELEA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA.

2025-06-20 19:25:17
Cover photo

Benki Kuu ya dunia (WB) kupitia Dkt. Lucy Ssendi ambaye Ni mtaalamu wa mabadiliko ya hali ya hewa wametembelea Chuo Cha Serikali za Mitaa Kampasi Kuu Hombolo na kukutana na viongozi wa Chuo wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Lameck Yusuph Mashala.

Viongozi hao kutoka pande zote mbili wakiwakilisha taasisi zao, wamekutana Leo Juni 20, 2025 na kufanya kikao katika ukumbi Mdogo wa mikutano kilichotengeneza ushirikiano chanya katika kusukuma gurudumu la Maendeleo kwa Jamii kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa mpaka Serikali Kuu.

Kikao hicho kililenga hasa uanzishwaji wa mradi wa Utafiti wa Majaribio (Pilot Study) wa kutoa mafunzo ya muda mfupi juu ya Mazingira ya Afya ya Jamii na Usimamizi wa Usalama na Viatarishi kwa makundi lengwa Kama Maafisa, Mazingira, Maafisa Maeneeleo ya Jamii, Maafisa Kilimo, Maafisa Afya ya Jamii, na Wachimbaji Ngazi ya chini hasa kokoto na mchanga.

Mradi huu utaendeshwa kwa kushirikisha taasisi husika zitakazotoa wataalamu kwa kila eneo husika kama vile DOSH, NEMC, na OSHA watakaoshirikiana na Wanataaluma kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa.

Akiongea wakati wa ugeni huo kutoka Benki ya Dunia Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Dkt. Mashala ameishukuru Benki hiyo kwa mchango wao mkubwa kwa kuweza kufadhili mradi huo utakaoanza kutekelezwa hivi karibuni baada ya mipango na mikakati ya awali kukamilika chini ya Chuo Cha Serikali za Mitaa.

Benki Kuu ya Dunia kupitia Chuo Cha Serikali za Mitaa itafadhili mradi huo utakaoanza kuendeshwa Kwa hatua za awali Kama mradi wa utafiti wa majaribio kwa kipindi kama itakavyopangwa katika mpango Kazi utakaoandaliwa hivi karibuni.

<