• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
The Local Government Training Institute (LGTI)
The Local Government Training Institute (LGTI)

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government The Local Government Training Institute (LGTI)

  • Home
  • About Us
    • Organization Structure
    • Vision and Mission
    • Objectives
    • Core Values
  • Administration
    • Board of Trustees
    • Office of the Rector
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Public Relations Unit
      • Information and Communication Unit
      • Deputy Rector PFA
        • Dean Of Students
        • Director Of Human Resource and Administration
        • Director Of Finance and Accounts
        • Director Of Planning and Institution Dev
          • Department Of Estate Management
        • Director Of Health
      • Deputy Rector ARC
        • Director Of Research and Consultancy
        • Registrar
        • Director Of Quality Assurance
        • Director Of Studies
  • Academics
    • Student Information System (SIS)
    • Student Information System (For Bachelor II and III)
    • Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki (MUKI)
      • Student Information System (SIS)
    • Department of Research, Short Course and Consultancy
    • Department of Human Resource Management
    • Department of Community Development
    • Department of Local Government Administration and Management
    • Department of Local Government Accounting and Finance
    • Department of Coordination and Quality Assurence
  • Admission
    • Maombi kwa njia ya Mtandao
    • Confirm Admission(Bachelor)
    • Programs Offered
    • Entry Qualifications
    • Fee Structure
    • Prospectus
    • Joining Instructions
  • Students Welfare
    • Student Information System (SIS)
      • New menu item
    • Dean Of Students
    • LOGISO
    • Hostels
    • Students By-laws
    • Campus Life
    • Almanac
    • Appeal Form
  • Publications
    • Reports
    • Journals
    • Acts
    • Press Release
  • Media Centre
    • Video Gallery
    • Photo Gallery
  • Maombi kwa njia ya Mtandao

LGTI yang’ara michezo ya SHIMIVUTA 2021

Posted on: December 19th, 2021

Wanamichezo wa Chuo Cha Serikali za Mitaa (LGTI) walioshiriki michezo ya 46 ya Shirikisho la Michezo la Vyuo vya elimu ya juu Tanzania (SHIMIVUTA) wamefanya vizuri katika michezo mbalimbali inayoandaliwa na Shirikisho hilo yaliyofikia kilele chake jana Jumamosi tarehe Disemba 18, 2021 katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Akitoa hutoba yake kwa waratibu, washiriki na wananchi mbalimbali waliohudhuria mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Moyo aliwapongeza wote waliamua kufanya mashindano ya mwaka huu mkoani Iringa na kuwaomba waandaji hao kwa mwaka 2022 mashindano hayo yafanyike tena mkoani Iringa kwani kuwepo kwa mashindano hayo kumeufanya mkoa wa Iringa kuchangamka kwa shughuli za michezo na kiuchumi na pia kumetoa fursa kwa vyuo mbalimbali kujitangaza hasa katika ukanda wa nyanda za juu kusini.

“Ndugu waandaji na washiriki wote wa michezo ya SHIMIVUTA mwaka 2021 nna uhakika kwa kukaa kwenu katika mkoa wa Iringa kwa kipindi cha Zaidi ya wiki mmekuwa salama na mmefurahia mazingira ya mkoa wa Iringa na pia mmepata fursa ya kujitangaza na kuwahamasisha vijana wetu wenye nia ya kupata elimu kuja kujiunga na vyuo vyenu kwani leo hii wamejionea jinsi Tanzania ilivyokuwa na idadi kubwa ya vyuo na kujua kuwa vyuoni mbali masomo mbalimbali yanayofundishwa kumbe pia kuna fursa ya kushiriki katika michezo kwani kwa sasa michezo ni ajira, ningetamani na mwaka 2022 mashindano haya yafanyike tena mkoani Iringa” Alisema Mhe. Moyo.   

Akitangaza zawadi mbalimbali zilizoshindaniwa tangu mwanzo wa mashindano hayo Mjumbe wa kamati tendaji wa michezo ya SHIMIVUTA ambaye pia ni Mwalimu wa michezo kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa bwana Ashraf Athumani alisema kwa mwaka 2021 LGTI  kimechukuwa ushindi wa jumla katika mchezo wa mpira wa pete (Netball) kwa kushika nafasi ya kwanza na kushika nafasi ya pili katika mchezo wa riadha ambapo mshindi wa kwanza kilikuwa Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP).

Akizungumzia namna mashindano hayo yalivyoandaliwa hadi kufikia tamati Mwalimu huyo wa michezo alisema kwa mwaka huu kuna baadhi ya vyuo havikushiriki lakini mwakani watajitahidi kupeleka mialiko mapema ili ile dhana ya vyuo vya elimu ya juu ionekane kwa kila Chuo kushiriki.

“Tangu tarehe 9/12 mashindano yalivyoanza mpaka leo tarehe 18 mashindano yamekuwa ya mafanikio sana na wanamichezo wote wameonesha uwezo wao kwa kushiriki katika michezo mbalimbali na hatimaye mabingwa wamepatikana na sisi kama waratibu tutajitahidi kuhakikisha mwakani vyuo vingi vinashiriki ili kuongeza hamasa na ushindani” Alisema bwana Ashraf.

Wakionekana wenye furaha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wamefurahishwa na mashindano hayo na kusema pamaoja na kushiriki michezo lakini pia kumewapa fursa ya kubadilisha mazingira na kuongeza marafiki kutoka vyuo tofauti vilivyoshiriki.

“Tumefurahi kuja Iringa na kushiriki mashindano haya ya SHIMIVUTA na tunaomba mwakani waandaji waalike vyuo vingi ili ushindani uwepo” Alisena Abdulrahman Shekh Abdallah Mwanafunzi kutoka Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)

Kwa upande wao Teresia Nicolaus Umuri aliyeshinda nishani (medali) nne za dhahabu katika riadha na Suzana Japhet nahodha wa mchezo wa pete (Netball) kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa wameeleza furaha yao kwa kushiriki na kushinda nafasi ya kwanza katika michezo hiyo na kuahidi kutetea nafasi zao katika mashindano ya mwakani.

Katika mashindano ya mwaka huu mabingwa katika mchezo wa mpira wa miguu ni Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT),mshindi wa pili ni Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) na Mshindi wa Tatu ni Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mpira wa pete (Netball) Mshindi wa kwanza ni Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), mshindi wa pili ni Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) na mshindi wa tatu ni Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) katika mpira wa kikapu mshindi wa kwanza ni Chuo Cha Elimu ya  Biashara (CBE), mshindi wa pili ni Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na mshindi wa tatu ni chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa upande wa mpira wa wavu  wanaume mshindi wa kwanza ni Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), mshindi wa pili ni Taasisi ya Teknolojia Dar es salam (DIT) na mshindi wa tatu ni Taasisi ya Uhasibu Arusha (AIA) na mpira wa wavu wanawake mshindi ni wa kwanza ni Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, mshindi wa pili ni Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA) na mshindi wa tatu ni Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT).

Mashindano hayo vilevile yameshuhudiwa zikitolewa nishani (medali) mbalimbali  kwa washindi wa riadha kuanzia mita 100 hadi mita 1500 na mbio za kupokezana vijiti, wachezaji bora katika michezo yote na vyeti vya ushiriki kwa kila Chuo.

Mwaka huu 2021 mashindano ya SHIMIVUTA yameshirikisha vyuo 14 ambavyo ni Chuo Cha Serikali za Mitaa (LGTI), Kituo Cha Mahusiano ya Nje (CFR),Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam(DIT),Chuo Cha Elimu ya  Biashara (CBE), Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE),Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT),Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP),Chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA),Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA),Chuo Cha Maji (WI), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na  Taasisi ya Ustawi wa Jamii na kwa mwaka 2022 mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza.

Announcements

  • APPROVED EXAMINATION RESULTS FOR SEMESTER I Academic Year 2022/2023 March 31, 2023
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALICHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KWA MKUPUO WA MACHI (MARCH INTAKE) 2022/2023 March 21, 2023
  • View All

Latest News

  • BARAZA LA WAFANYAKAZI LGTI LAPATIWA MAFUNZO

    December 30, 2022
  • LGTI BINGWA NETBALL VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA

    December 20, 2022
  • CCM DODOMA MJINI WAFUNDWA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA

    December 10, 2022
  • 4923 Wahitimu Chuo Cha Serikali za Mitaa 2022

    December 01, 2022
  • View All

Video

Heri ya Pasaka
More Videos

Quick Links

  • TCU Admission Almanac for 2021/2022 Admission Cycle
  • Student By-laws
  • OPRAS Forms
  • Institute's Almanac
  • Prospectus

Related Links

  • Tamisemi
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Public Service Recruitment Secretariat

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Hombolo

    Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania

    Telephone: +255 26 296 1101

    Mobile: 733542917/733542915

    Email: info@lgti.ac.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Ghostwriter

    • Disclaimer
    • Privacy Policy

Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.