- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza wa mwaka wa masomo 2022/2023 kuanzia leo Julai 8,2022 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita.
Katibu Mtendaji wa TCU,Prof.Charles Kihampa amesema dirisha litakuwa wazi hadi Agosti 5,2022 na kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU au tovuti za Vyuo mbalimbli vinavyotoa elimu ya juu.
Waombaji wote wa udahili wa kwa mwaka wa masomo 2022/2023 wanatakiwa kuwa na sifa stahiki za kidato cha sita, sifa stahiki za Stashahada na Cheti cha awali.
Kwa waombaji wenye vyeti vilivyotolewa na mabaraza ya mitihani nje ya nchi ni lazima wawasilishe vyeti vyao Baraza la Mitahani la Tanzania.
Waombaji kwa ngazi ya Shahada ya awali mnaweza kuomba udahili kwenye fani za Maendeleo ya Jamii,Utawala katika Serikali za Mitaa na Rasilimali watu katika Chuo cha Serikali za Mitaa kupitia online Application System inayopatikana kwenye tovuti ya Chuo www.lgti.ac.tz
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.