- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Chuo cha Serikali za Mitaa kinaendelea kutoa mafunzo kwa Kamati za Fedha,Utawala na Uongozi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa inayojumuisha Mikoa ya Shinyanga,Iringa,Dodoma na Tabora ili kuzijengea uwezo kamati hizo. Mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo yaliyofanyika wiki iliyopita katika mikoa ya Arusha na Morogoro ambayo ni kutekeleza maelekezo yaliyotolewa katika kikao kazi cha Msajili wa Hazina na wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 mpaka 21 Agusti 2023.
Akitoa mada ya kwanza ya Msingi wa kisheria na majukumu ya kamati za fedha Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa Petro Nziku aliwashauri waheshimiwa wajumbe wa kamati hizo kila wanapokutana kuzijadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na kukagua baadhi ya vyanzo vya mapato katika Halmashauri zao ili Halmashauri hizo ziweze kuongeza mapato yao.
Zingine zilizotolewa katika siku ya kwanza ni nafasi ya kamati za fedha katika utungaji wa sheria ndogo na usimamizi wa rasilimali watu, ajira na nidhamu.
Pamoja na Mafunzo hayo kufanyika mkoani Dodoma kwa mikoa ya Shinyanga,Iringa,Dodoma,Singida na Tabora mafunzo kama hayo pia yanafanyika Katika mkoa wa Mwanza kwa mikoa ya Kigoma,Geita,Kagera,Mara, Simiyu na Mwanza na katika mkoa wa Mbeya yanajumuisha mikoa ya Njombe,Songwe,Rukwa,Katavi,Ruvuma na Mbeya.
Chuo cha Serikali za Mitaa kimekuwa chuo kiongozi kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa mamlaka zote za Serikali za Mita na Ofisi mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa vijana wanaohitimu kidato cha nne na sita kuanzia ngazi ya Astashahada mpaka shahada ya awali.
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.