- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Maafisa mipango na wachumi nchini Tanzania wametakiwa kujikita katika uandishi wa miradi na kubuni njia mbadala za kusaidia kugharamia miradi itakayozalisha mapato na kuhakikisha wanapanga mipango na kuitekeleza katika mamlaka zao ili kuweza kubadilisha takwimu na kuleta maendeleo.
Hayo yamesemwa leo tarehe 28 Septemba Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bwana John Cheyo alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Maafisa Mipango na Wachumi kutoka katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Halmashaurizote Tanzania yanayotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa.
“Ndugu zangu wachumi mliokutana hapa, haya mafunzo ni muhimu sana kwenu, zingatieni mafunzo haya kwa kujadiliana changamoto mbalimbali ili mkazitatue na mkalete mabadiliko kwa mamlaka mlizotoka” Alisema Bwana Cheyo
Mkurugenzi huto pia aliwataka wachumi hao kuhakikisha hela zilizotumwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zinasimamiwa ipasavyo na zitumike kwa miradi husika.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ametoa shilingi bilioni mia moja sitini kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nchi nzima, mara baada ya kutoka hapa mkasimamie madarasa hayo yajengwe katika ubora na viwango bora kwani hatutaki kusikia wanafunzi wamebaki nyumbani kwa ukosefu wa madarasa.
Pamoja na kuongea na wachumi hao vilevile Bwana Cheyo alimtaka Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa kuhakikisha wanakwenda katika mikoa yote kutoa mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na watumishi wote waliopo katika mamlaka hizo kwani Chuo hicho kilianzishwa kwa madhumuni ya kushughulikia mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akiongea kabla ya kumkarisha Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Dkt.Lameck Mashala alisema lengo la mafunzo hayo kwa wachumi ni kuongeza uelewa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akitoa neon la shukurani Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia fedha na mipango Dkt. Lazaro Kisumbe pamoha na kushukuru kwa niaba ya Mkuu wa Chuo waliahidi kuyatekeleza yote aliyoyaelekeza na kumpa mrejesho namna walivyotekeleza.
Mafunzo hayo ya siku tatu kwa wachumi ni muendelezo wa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi yanayoendelea kutolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa kwa taasisi za Serikali na sekta binafsi.
Pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Serikali za Mitaa pia kinatoa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Asstashahada ya awali hadi stashahada katika fani za Utawala katika Serikali za Mitaa,Maendeleo ya Jamii,Ugavi na manunuzi, Rasilimali watu,Utunzaji wa kumbukumbu na Nyaraka na Uhasibu pia Chuo kinatoa shahada katika fani za Maendeleo ya Jamii,Utawala katika Serikali za Mitaa na Rasilimali Watu.
Kwa Picha mbalimbali za matukio angalia kwenye Maktaba ya picha.
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.