- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Baraza la Wafanyakazi la Chuo cha Serikali za Mitaa limekutana leo Alhamisi tarehe 01/10/2020 chuoni Hombolo. Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi alisisitiza kuwa baraza ni chombo muhimu katika kusimamia mustakabali wa taasisi, hivyo wajumbe washiriki kwa kujadili na kutoa hoja zitakazosaidia kuimarisha ustawi wa taasisi.
"Chuo chetu kinatekeleza majukumu mengi yanayochangia ustawi wetu kama watumishi, ustawi wa Chuo chetu na taifa kwa ujumla. Hivyo, mijadala yetu ilenge tija kuelekea kuboresha na kuimarisha ustawi wa taasisi yetu na watumishi wake"
Kikao hicho kilipokea na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya taasisi kutoka katika idara na vitengo mbalimbali. Katika ya taarifa hizo ilitolewa Taarifa ya Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu ambayo iliwasilisha masuala ya udahili wa wanafunzi wapya takriban 7600 kwa mwaka wa masomo 2019/2020, tafiti zilizo kamilika na kuchapishwa, na mafunzo ya muda mfupi yaliyotolewa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Vilevile, Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala Mipango, na Fedha aliwasilisha taarifa mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kwa watumishi, stahiki mbalimbali zilizotolewa kwa watumishi na upandishaji vyeo watumishi.
Wajumbe wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi wa tawi na wa kitaifa pia walishiriki katika kikao hicho muhimu kwa ustawi wa Chuo na watumishi wake.
Picha mbalimbali za wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia mijadala katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.