- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Chuo cha Serikali za Mitaa leo kimeanza rasmi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa katika kikao kazi cha Msajili wa Hazina na wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 mpaka 21 Agusti 2023.
Mafunzo hayo kwa kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa yameanza kutolewa leo kwa kanda ya nne inayojumuisha mikoa ya Mtwara,Lindi,Pwani, Dar es Salaam Morogoro na Halmashauri ya Kilolo kutoka mkoa wa Iringa ambayo yanafanyika Mkoani Morogoro na kanda ya tano hufanyika mkoa wa Arusha ambayo inajumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Manyara na Tanga.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe.Rebeka Nsemwa aliwataka Waheshimiwa Madiwani wote waliopo katika kamati za Fedha,Mipango na Utawala kuzingatia mafunzo hayo na kwenda kuyatumia vizuri ili kuleta maendeleo katika halmashauri wanazozihudumia kwa kuzinagatia kuwa kamati hizo ndio roho ya maendeleo ya Halmashauri zao.
“Waheshimiwa Madiwani, nyinyi ndio wasimamizi wakuu wa Halmashuri zenu katika kukusanya mapato na kusimamia miradi iliyomo kwenye Halmashauri zenu, kwa hiyo yatumieni mafunzo haya kwa kuhakikisha mnakuwa wasimamizi wakuu wa halmashauri mnazotoka ili wananchi wenu waone kuwa kweli madiwani mnawajibika” Alisema Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.
Pamoja na kuwataka Waheshimiwa Madiwani hao kuzisimamia Halmashauri zao lakini pia Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kumtaka Mkuu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatoa mafunzo hayo kwa weledi wa hali ya juu ili ile dhana ya kuonekana kuwa Chuo Cha Serikali za Mitaa ni Chuo kiongozi kwa kutoa mafunzo kwa mamlaka za Serikali za Mitaa na kuwataka pamoja na kutoa mafunzo kwa Kamati za Fedha,Mipango na Uongozi pia waandae mafunzo kwa kamati zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa na hata baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwaka 2024.
Akiongea kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Daktari Michael Msendekwa alisema kuwa mafunzo hayo yamegawanywa katika kanda tano kwa lengo la kuwawezesha watoa mada kutoa mafunzo hayo kwa makundi madogo madogo ili kuleta ufanisi kwa wajumbe watakaoshiriki.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi tumeyagawa mafunzo haya katika kanda tano tofauti ili iwe rahisi kwa wawezeshaji wetu kutoa mafunzo vizuri kwani wataweza kuhudumia kwa kutoa mada na kuweza kuongeza usikivu na umakini kwa waheshimiwa Wajumbe wa kamati ya Fedha,Mipango na Uongozi, na nikuhakiksihie Mheshimiwa Mgeni Rasmi mafunzo haya yatatolewa kwa usawa kwa kanda zote ili waheshimiwa wote wawe na uelewa wa Pamoja” Alisema Kaimu Mkuu wa Chuo
Mafunzo hayo yamegawanywa katika kanda tano ambazo ni kanda ya kwanza inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Iringa,Dodoma,Singida na Tabora Mafunzo yatafanyika Mkoani Dodoma, Kanda ya pili ina mikoa ya Kigoma,Geita,Kagera,Mara, Simiyu na Mwanza Mafunzo yatafanyika Mkoani Mwanza,Kanda ya tatu inajumuisha mikoa ya Njombe,Songwe,Rukwa,Katavi,Ruvuma na Mbeya mafunzo hayo yatafanyikia Mkoni Mbeya wakati kanda ya nne inajumuisha mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani,Dar es salaam na Morogoro na kwa kanda ya tano inajumuisha mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Manyara na Tanga.
Chuo cha Serikali za Mitaa kimekuwa chuo kiongozi kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa mamlaka zote za Serikali za Mita na Ofisi mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa vijana wanaohitimu kidato cha nne na sita kuanzia ngazi ya Astashahada mpaka shahada ya awali.
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.