- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Majina ya awamu ya kwanza ya Wanafunzi kwa wanafunzi waliomba kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Masomo 2023/2024 yametangazwa leo Jumatatu ili wanafunzi wote waliochaguliwa waanze maandalizi ya kujiunga na Chuo ifikapo Tarehe 16 Mwezi wa kumi, 2023.
Akitangaza majina hayo Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma Daktari Michael Msendekwa amesema kuwa majina hayo yametangazwa kwa mujibu ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Stadi (NACTVET) na kuwataka Wazazi, Walezi na wanafunzi ambao majina yao hayapo kwenye orodha hiyo iliyotangazwa wasiwe na wasiwasi kwani majina yao yataonekana kwenye majina yatakayotangazwa katika awamu ya pili na ya tatu kwani mpaka sasa bado watu wenye uhitaji wanaendelea kufanya maombi.
"Nawasihi sana wale wote ambao majina yao hayamo kwenye orodha iliyotangazwa leo wasiwe na wasiwasi wowote na tunawahakikiashia wote walioomba na wana sifa watapata nafasi ya kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa" Aliongeza Daktaru Msendekwa.
Akizungumzia juu ya namna ya kulipa Ada Naibu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Daktari Lazaro Kisumbe amewataka wazazi kuwa watulivu kwani utaratibu wote wa kulipia kila aina ya malipo wataupata kupitia tovuti hii na njia mbalimbali za mawasiliano kupitia namba zao za simu walizoandika wakati wa kufanya maombi.
Kuangalia majina hayo Tafadhali bonyeza hapa Awamu ya kwanza.pdf
Pia unaweza kupakua fomu yenye maelekezo ya Chuo hapa Fomu ya kujiunga na Chuo.pdf
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.