- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Wanafunzi 4923 wamehitimu mafunzo yao katika ngazi mbalimbali Chuo cha Serikali za Mitaa kwa mwaka 2022 na kutunukiwa Astashahada,Stashahada na Shahada ya awali katika mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo siku ya Alhamis tarehe 1 Disemba,2022.
Akiongea wakati wa mahafali hayo Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo hicho Prof.Joseph Kuzilwa aliwataka wahitimu kuzingatia masomo waliyofundishwa na kuyatumia vizuri ili yalete tija kwa jamii zinazo wazunguka.
"Ndugu wahitimu leo mnamaliza masomo yenu katika ngazi mbalimbali, kaitumieni elimu mliyopata kuleta manufaa kwa jamii na kuziletea maendeleo jamii zenu na mkawe mabalozi wazuri wa Chuo huko muendako" Alisema Prof.Kuzilwa
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Dkt. Mashala Yusuph aliwapongeza wahitimu hao kwa kumaliza masomo yao na kuwataka wale ambao wamemaliza Astashahada kuendelea na Stashahada na wahitimu wa Stashahada wasiache kurudi chuoni hapo kuendelea na ngazi ya Shahada ya awali (Digrii) kwani kwa sasa Chuo kimejenga miundombinu ya kisasa ya madarasa, mabweni pamoja na walimu wa kutosha.
Mahafali hayo yalitanguliwa na Kongamano la Wanataaluma lililofanyika Chuoni hapo likiongozwa na Naibu Katibu Mkuu- TAMISEMI Ramadhani Kailima na kugawa zawadi na vyeti mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vyema katika masomo.
Kwa picha mbalimbali za Siku ya Mahafali na Kongamano la Wanataaluma tembelea Kituo cha Habari (Media Center) kisha angalia Maktaba ya Picha (Photo Gallery)
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.