- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Serikali imevitaka vyuo vyote nchini kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea ruzuku ya fedha za matumizi kutoka Serikali kuu.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Deogratius Ndejembi alipomuawakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa katika Mahafali ya 15 ya Chuo Cha Serikali za Mitaa (Hombolo) .
“Chuo hiki kina hazina ya wabobezi wa fani mbalimbali, fanyani tafiti na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kupunguza utegemezi, vilevile endeleeni kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo na shughuli nyinmgine zinazohusu ustawi wa chuo” Alisema Mhe.Ndejembi.
Mhershimiwa Ndejembi pia alisema azma ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alifanya kikao na watendaji wa Taasisi mbalimbali nchini mwezi Agosti,2023 ni kuona mashirika ya Umma yanaongeza tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kupunguza utegemezi wa rusuku kutoka mfuko wa Serikali Kuu.
“Mashirika na Taasisi za Serikali ziendelee kubuni mikakati ya kuongeza mapato ili faida itumike kuendesha shughuli za Taasisi na kutoa gawio kwa Serikali,maelekezo haya pia yalihusu jumuiya ya chuo hiki,ongezeni kasi ya kuibua mikakati inayotekelezeka na yenye tija” Alisisitiza Mhesimiwa Naibu Waziri Ndejembi.
Akijibu kuhusu kero ya Barabara ya kutoka Ihumwa hadi Hombolo Mheshimiwa Ndejembi alisema tayari upembuzi yakinifu umeshafanywa pia amewaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kazi ianze kwa wakati baada ya kukamilika kwa taratibu zote.
Akisoma risala kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chuo Cha Serikali za Mitaa Prof. Joseph Kuzilwa alitoa ombi la kupatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo pacha ya kampasi ndani ya Jiji la Dodoma baada ya kupata eneo la ilipokuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuondokana na adha ya kukodi kwani upembuzi yakinifu juu ya majengo hayo tayari umefanmyika lakini tatizo ni ufinyu wa bajeti.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa Dkt.Mashala Yusuph alisema Chuo hicho kimepewa jukumu la kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, kufanya tafiti na kutoa ushauri elekezi ambapo mpaka sasa kwa upande wa mafunzo ya muda mrefui chuo kinatoa mafunzo katika fani sita ambazo ni Utawala na Uongozi katika Serikali za Mitaa,Maendeleo ya Jamii,Utawala na Rasilimali Watu,Utunzaji kumbukumbu na Nyaraka,Ugavi na manunuzi na Uhasibu na Fedha.
Kwa upande wake Mlau wa Chuo hicho Dkt.Danford Sanga amesema kuwa jumala ya wanafunzi 4,666 wamehitimu katika mahafali hayo ya 15 tangu chuo hicho kianze kutoa mafunzo ya muda mrefu mwaka 2007 kwa ngazi za Astashahada ya awali na kwamba matarajio ya Chuo ni kuona wahitimu hao wanatoa huduma bora kwa jamii zinazowazunguka.
Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Cha Serikali za Mitaa Bwana Stephen Thomas alitoa ombi la kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa kwa vyuo vingine vya kati ili waweze kujikimu katika masomo yao kwani wanafunzi walio wengi wanatoka katika mazingira magumu na familia zenye kipato cha chini na kupewa kipaumbele katika ajira kwani Chuo hicho ni Chuo pekee kilicho chini ya Wizara ya TAMISEMI.
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.