- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajia kuwaongoza wahitimu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa katika mahali ya kumi na tano ya Chuo hicho mnamo tarehe 07 Desemba, 2023 katika viwanja vya Chuo Kampasi kuu Hombolo.
Akiongea juu ya mahafali hayo Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Dkt.Yusuph Mashala amesema kuwa maandalizi yote kuhusu mahafali hayo yamekamilika na kuwataka wahitimu na wananchi wote kuhudhuria mahafali hayo bila kukosa.
"Mahafali ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake kwani tunatarajia kupokea wageni wengi wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa hivyo wahitimu na wananchi wote hakikisheni mnafika katika viwanja vya mahafali mapema kabla ya Mgeni rasmi hajafika ili wote kwa pamoja tuweze kumpokea mgeni wetu" Alisema Mkuu wa Chuo.
Mhafali hayo yatatanguliwa na Kongamano la wanataaluma litakalofanyika Chuoni hapo siku ya Jumatano tarehe 6 Desemba,2023 na kuongozwa na Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw.Adolf Ndunguru.
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.