- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Cha Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Masomo 2023/2024 wametakiwa kuanza mchakato wa kujitengenezea CONTROL NUMBER ili waanze kufanya malipo mapema kabla ya siku ya kuripoti chuoni hapo tarehe 16 Oktoba,2023.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Michael Msendekwa alipokuwa akitoa maelezo namna Chuo kilivyojipanga kwa ajili ya kuanza Mwaka mpya wa masomo 2023/2024 na kuwataka Wazazi/Walezi na wanafunzi kuhakikisha wanajitengenezea CONTROL NUMBER wenyewe kupitia Simu zao (Smart phones) au kwenda kwa watoa huduma za Internet ili waweze kupata CONTROL NUMBER ili waanze kufanya malipo kabla ya kuripoti.
"Chuo chetu ni chuo cha Serikali kwa hiyo malipo yote ni lazima yafanyike kwa kupitia mifumo rasmi ya Serikali kwa hiyo nawaasa kujipatia Control Number za Malipo ya Ada kwenye tovuti yetu mapema ili Mzazi/Mlezi aanze kulipa kwa awamu kwani Control Number hiyo inaruhusu kupokea malipo kwa awamu hadi utakapomaliza ada yako ndani ya mwaka mmoja wa masomo" Alisema Dkt.Msendekwa.
Kaimu Mkuu huyo wa Chuo amesisitiza kuwa malipo yote yafanyike kwa kutumia Benki za CRDB, NMB, Wakala na Mitandao ya Simu (TigoPesa,Airtel Money au Mpesa) na kuwataka kutunza risiti na kuja nazo Chuoni kwa ajili ya uthibitisho wa malipo.
"Control Number hizo zitakuwa kwa ajili ya malipo ya Ada na Serikali ya Wanafunzi tu, kwa malipo ya Malazi (Hostel) na BIMA ya Afya kila mwanafunzi atapata maelekezo mara baada ya kufika Chuoni" Kaimu Mkuu wa Chuo aliongeza.
Dkt.Msendekwa amewatahadharisha wazazi na walezi kuwa hakuna malipo yatakayofanyika nje ya utaratibu wa chuo kwa hiyo ni vema wazazi wakawa waangalifu ili wasitapeliwe na matapeli kwani Chuo hakitahusika na utapeli wa aina yoyote.
Control Number hizo zimeanza kutoka leo kwa wale wanafunzi wote waliochaguliwa na Serikali na wale walioomba na majina yao kutoka katika awamu ya kwanza na pia kwa wale ambao majina yao yatatoka katika awamu ya pili na awamu ya tatu watatumia utaratibu huohuo wa kupata Control Number na kufanya malipo.
Zifuatazo ni hatua za kupata CONTROL NUMBER
Hatua ya Kwanza
Hatua ya PiliHatua ya TatuHatua ya NneHatua ya Tano
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.