- Home
- About Us
- Organization Structure
- Board of Trustees
- Rector
- Gallery
- Publications
- Students Welfare
- Campuses
Viongozi kutoka Chama cha Mapinduzi wa kata zote 41 za Dodoma mjini wamepatiwa mafunzo mara baada uchaguzi wa ndani ya chama ulioanza mwaka huu kuanzia ngazi ya matawi,kata,wilaya,mikoa na kuhitimishwa na ngazi ya Taifa uliofanyika siku ya Alhamisi.
Akiongea wakati akifungua mafunzo hayo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Mhe. Donald Mejetii aliwataka viongozi hao kuzingatia mafunzo hayo ili kuhakikisha Chama kinaanzisha na kusimamia miradi mbalimbali.
“Ilani ya CCM ndio inayotekelezwa na serikali na sisi viongozi ndio watekelezaji wakuu wa ilani hiyo ndo maana hawa chuo cha Serikali za Mitaa wakaona ni vema watuongezee ujuzi kwa sababu nyinyi huko mlipo ndio mpo na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata na matawi,sisi tukiridhika maana yake tunapeleka taarifa ngazi ya juu kuwa kazi inakwenda vizuri kwa hiyo naomba baada ya kupata mafunzo haya mkasimamie ilani kwa watumishi wetu”
Akiwakaribisha wageni Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Dkt. Mashala Yusuph aliwataka viongozi hao kuzingatia mafunzo watakayoyapata kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa ili kuwa viongozi tofauti na viongozi ambao hawajapata mafunzo.
“Ndugu zangu viongozi wa Chama Mkoa kata zote za Dodoma,Nawaomba mukayatumie mafunzo haya kwa ufanisi ili kuwaletea maendeleo wanachama wenu na wananchi kwa ujumla na pia nawaomba kila mkipata nafasi msiache kuja kupata mafunzo chuoni kwetu kwani chou chetu kinatoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi” Alisema Dkt. Mashala.
Akizungumzia juu ya mafunzo ya muda mrefu Mkuu huyo wa Chuo aliwataka viongozi hao kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao ya utawala kwa kuwahamasisha wazazi na walezi kuwaleta vijana wao kuja kupata elimu katika Chuo cha Serikali za Mitaa.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zilifundishwa kama Uandishi wa Muhtasari na utunzaji wa kumbukumbu,Ujasiriamali Siasa itikadi na uenezi katika Chama na mada ya Upembuzi wa Ilani ya Chama.
Chuo cha Serikali za Mitaa kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi kwa Taasisi za Serikali, Taasisi binafsi, Vyama vya kisiasa na makundi mbalimbali na pia chou hicho kinatoa mafunzo ya muda mrefu kuanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada katika fani mbalimbali kama Utunzaji kumbukumbu na Nyaraka,Utawala katika Serikali za Mitaa,Utawala na Rasilimali watu, Ugavi na Manunuzi,Maendeleo ya Jamii na Uhasibu na Fedha na kwa upande wa Shahada ya awali Chuo kinatoa mafunzo katika fani za Maendeleo ya Jamii, Utawala katika Serikali za Mitaa na Utawala na Rasilimali Watu.
Kwa picha mbalimbali za mafunzo hayo tembelea Kituo cha Habari (Media Center) kisha angalia Maktaba ya Picha (Photo Gallery)
Hombolo
Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania
Telephone: +255 0652870635
Mobile: +255 0652870635
Email: info@lgti.ac.tz
Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.