• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff email |
Local Government Training Institute (LGTI)
Local Government Training Institute (LGTI)

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Local Government Training Institute (LGTI)

  • Home
  • About Us
    • Organization Structure
    • Vision and Mission
    • Objectives
    • Core Values
  • Administration
    • Board of Trustees
    • Office of the Rector
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Public Relations Unit
      • Information and Communication Unit
      • Deputy Rector PFA
        • Dean Of Students
        • Director Of Human Resource and Administration
        • Director Of Finance and Accounts
        • Director Of Planning and Institution Dev
          • Department Of Estate Management
        • Director Of Health
      • Deputy Rector ARC
        • Director Of Research and Consultancy
        • Registrar
        • Director Of Quality Assurance
        • Director Of Studies
  • Academics
    • Student Information System (SIS)
    • Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki (MUKI)
      • Student Information System (SIS)
    • Department of Research, Short Course and Consultancy
    • Department of Human Resource Management
    • Department of Community Development
    • Department of Local Government Administration and Management
    • Department of Local Government Accounting and Finance
    • Department of Coordination and Quality Assurence
  • Admission
    • Online Application System (OAS)
    • Confirm Admission(Bachelor)
    • Programs Offered
    • Entry Qualifications
    • Fee Structure
    • Prospectus
    • Joining Instructions
  • Students Welfare
    • Student Information System (SIS)
      • New menu item
    • Dean Of Students
    • LOGISO
    • Hostels
    • Students By-laws
    • Campus Life
    • Almanac
    • Appeal Form
  • Publications
    • Reports
    • Journals
    • Acts
    • Press Release
  • Media Centre
    • Video Gallery
    • Photo Gallery
  • Online Application System (OAS)

Waziri TAMISEMI atoa ahadi ya ujenzi wa bweni Hombolo

Posted on: November 26th, 2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) jana tarehe 25/11/2021 ametoa ahadi ya ujenzi wa bweni kwa mwaka wa fedha 2022/2023 katika Chuo Cha Serikali za Mitaa lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 2500 ili kuondoa tatizo la uhaba wa mabweni chuoni hapo.

Waziri Ummy ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wanafunzi na wananchi mbalimbli waliojitokeza  katika mahafali ya 13 ya Chuo Cha Serikali za Mitaa kilichopo Hombolo mkoani Dodoma.

“Haiwezekani Chuo kama hiki ambacho kipo chini ya Wizara yangu kuona wanafunzi wengi wanakaa nje ya chuo na kwa kuwa kila mwaka idadi ya wahitimu wanaongezeka kutoka wanafunzi  5751 mwaka 2019/2020 hadi wanafunzi 6021 kwa mwaka wa masomo 2020/2021, hali hii inaonyesha jinsi gani chuo hiki kilivyokuwa na umuhimu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kwa hiyo lazima tutenge fedha katika bajeti ijayo ili kuhakikisha tunapunguza changamoto ya malazi katika chuo hiki” Alsema Mheshimiwa Waziri Ummy.

Pamoja na ahadi ya bweni kwa wanafunzi Mheshimiwa Waziri pia alitoaha ahadi ya kulishughulikia tatizo la barabara na maji kwa luwasiliana na waziri wa ujenzi Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

“Nimesikia pia mmezungumzia tatizo la barabara na tatizo la maji hapa Hombolo,sasa haya masuala mawili niachini mimi nitakwenda kuongea na Waziri wa ujenzi Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa maji ili tulitatue hili tatizo kwa haraka” Alisisitiza Mheshimiwa Ummy.

Pamoja na ahadi hizo Mheshimiwa Waziri pia aliwasisitiza wanafunzi wa Chuo Cha Serikali za Mitaa kusoma kwa bidii na kuwa tayari kufanya kazi katika Halmashauri yoyote watakayopata kazi kwani kuna mtindo umeibuka kwa watumishi wapya kutaka kuhamia mijini mara wapatapo kazi kwa kisingizio cha kuwafuata wenza wao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Prof. Joseph Kuzilwa akiongea kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Mwenyekiti na kumuahidi yeye na wajumbe wenzake kuhakikisha wanamsaidia Rais majukumu ya kukisimamia Chuo kwa kufuata sheria na taratibu ili kukifanya kiwe chuo cha mfano kwa kutoa wahitimu wenye weledi nchini.

“Mheshimiwa Waziri nichukue nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa bodi, Namuahidi Mheshimiwa Rais mimi na wajumbe wa bodi tutatimiza majukumu yetu kwa ufanisi na kwa kufuata sheria na taratibu za Chuo” Alisema Profes Kuzilwa.

Akisoma hutuba kwa mgeni rasmi Mkuu wa Chuo Cha Serikali za Mitaa Daktari Mpamila Madale alimshukuru Waziri kwa kukubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, pamoja na kutoa shukrani zake Dkt. Madale pia alisema kuwa kwa sasa Uongozi wa Chuo umeshajenga madarasa ya kisasa pamoja na nyumba za walimu na jengo lingine la darasa lipo kwenye hatua ya msingi na pia wanaendelea kuyafanyia ukarabati baadhi ya madarasa na mabweni.

Mahafali hayo yalitanguliwa na kongamano la wanazuoni lililofanyika chuoni hapo siku ya jumatano tarehe 24/11/2021 likiwa na mada juu ya umuhimu wa sense ya watu na makazi zoezi ambalo linatarajia kufanyika mwaka 2022 nchi nzima.

Kongamano hili liliambatana na utoaji wa zawadi kwa walimu walioandika maandiko mbalimabli pamoja na  wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao.

Haya ni mahafali ya 13 ya Chuo Cha Serikali za Mitaa tangu chuo hicho kianzishwe na kwa sasa Chuo Cha Serikali za Mitaa kimeanza kutoa masomo kwa ngazi ya shahada za Maendeleo ya jamii na shahada ya Utawala na uongozi katika Serikali za katika.

Kwa picha mbalimbali za matukio ya kongamano la wanazuoni, uzinduzi wa bodi ya chuo na mahafali angalia kwenye maktaba ya picha/Photo gallery.

Announcements

  • Provisional Examination Results for Semester II Academic year 2021/2022 July 29, 2022
  • Maombi kwa njia ya Mtandao June 09, 2022
  • KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2022/23 January 24, 2022
  • Approved Examination Results for Supplementary,Special and Carry Over for Semester I Academic Year 2021/2022 April 25, 2022
  • View All

Latest News

  • TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI

    July 08, 2022
  • Dkt.Madale atembelea Banda la Chuo Sabasaba

    July 07, 2022
  • Karibuni LGTI kujiunga na Shahada kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023

    June 21, 2022
  • Maombi kwa njia ya Mtandao yarejea LGTI

    June 09, 2022
  • View All

Video

Mambo ya Mjomba kuhusu Chuo cha Serikali za Mitaa
More Videos

Quick Links

  • TCU Admission Almanac for 2021/2022 Admission Cycle
  • Student By-laws
  • OPRAS Forms
  • Institute's Almanac
  • Prospectus

Related Links

  • Tamisemi
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Public Service Recruitment Secretariat

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Hombolo

    Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania

    Telephone: +255 26 296 1101

    Mobile: 733542917/733542915

    Email: info@lgti.ac.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Ghostwriter

    • Disclaimer
    • Privacy Policy

Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.