• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff email |
Local Government Training Institute (LGTI)
Local Government Training Institute (LGTI)

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Local Government Training Institute (LGTI)

  • Home
  • About Us
    • Organization Structure
    • Vision and Mission
    • Objectives
    • Core Values
  • Administration
    • Board of Trustees
    • Office of the Rector
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Public Relations Unit
      • Information and Communication Unit
      • Deputy Rector PFA
        • Dean Of Students
        • Director Of Human Resource and Administration
        • Director Of Finance and Accounts
        • Director Of Planning and Institution Dev
          • Department Of Estate Management
        • Director Of Health
      • Deputy Rector ARC
        • Director Of Research and Consultancy
        • Registrar
        • Director Of Quality Assurance
        • Director Of Studies
  • Academics
    • Student Information System (SIS)
    • Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki (MUKI)
      • Student Information System (SIS)
    • Department of Research, Short Course and Consultancy
    • Department of Human Resource Management
    • Department of Community Development
    • Department of Local Government Administration and Management
    • Department of Local Government Accounting and Finance
    • Department of Coordination and Quality Assurence
  • Admission
    • Online Application System (OAS)
    • Confirm Admission(Bachelor)
    • Programs Offered
    • Entry Qualifications
    • Fee Structure
    • Prospectus
    • Joining Instructions
  • Students Welfare
    • Student Information System (SIS)
      • New menu item
    • Dean Of Students
    • LOGISO
    • Hostels
    • Students By-laws
    • Campus Life
    • Almanac
    • Appeal Form
  • Publications
    • Reports
    • Journals
    • Acts
    • Press Release
  • Media Centre
    • Video Gallery
    • Photo Gallery
  • Library

Wadau wa Nyumba za kulala wanafunzi Hombolo wakutana na Uongozi wa Chuo

Posted on: December 31st, 2021


Uongozi wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) leo umekutana na wamiliki na wasimamizi wa hosteli wanaofanya biashara ya kulaza wanafunzi wanaosoma chuoni hapo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu namna bora ya  kuzindesha na kuwa uelewa wa pamoja.

Akifungua kikao hicho Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Yusuph Mashala aliwaambia wadau hao kuwa ni muda mrefu  tangu Chuo kimefunguliwa kwa mwaka wa masomo 2021/2022 hawajakutana ndo maana kama uongozi wameamua kuwaita ili kujadiliana juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi kwa ustawi wa Chuo cha Serikali za Mitaa na jamii yote ya Hombolo kwa ujumla.

“Ndugu zangu wamiliki wa Hosteli nyinyi ni wadau wakubwa sana katika jamii yetu kwa kuwa Chuo chetu hakina uwezo mkubwa wa kuwapa huduma ya malazi wanafunzi wote na ndo maana asilimia kubwa ya wanafunzi wetu wanakaa nje kwa hiyo tumewaita hapa ili tujadiliane namna bora ya kuwasaidia wanafunzi waishi katika mazingira bora” Alisema Dkt.Mashala.

Pia Dkt.Mashala aliwataka wamiliki hao kuhakikisha wanafunzi wote wanaokaa kwenye hosteli zao wanakuwa na fomu za usajili wa chuo kwani mwanafunzi ambaye hajasajiliwa hatambuliki kama mwanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa.

“Ndugu zangu pia mkumbuke kuwa kuna madhara makubwa sana ya kukaa na mwanafunzi ambaye hana usajili na madhara ya kukaa na mwanafunzi asiyesajiliwa ni makubwa sana kiusalama” Aliongeza Kaimu Mkuu wa Chuo.

“Pamoja na kufanya biashara lakini pia lazima mjue nyinyi ni walezi wa hawa wanafunzi kwa hiyo tunahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwenu ili tuwalee kwa Pamoja” Alisisitiza Dkt.Mashala.

Akimkaribisa Kaimu Mkuu wa Chuo Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Bwana Askwar Niima alisema kuwa nia ya kuwaita wamiliki hao ni kupata majina kamili ya wamiliki na idadi ya hosteli zote binafsi na kuwaonyesha washauri wa wanafunzi wa hosteli za nje ili iwe rahisi kuwasiliana nao kwa jambo lolote linalotokea katika hosteli zao.  

Akizungumzia hali ya mlipoko wa magonjwa yanayoendelea Mganga mkuu wa Zahanati ya Chuo Bi.Neema Mkweji aliwataka wamiliki wa hosteli hizo kuhakikisha wanaweka ndoo za maji yenye dawa  ili wanafunzi wanawe mikono waingiapo na watokapo, wanatumia vitakasa mikono, kuwashauri wanafunzi kuvaa barakoa wakiwa sehemu zenye misongamano na kupunguza mlundikano wa wanafunzi wengi ndani ya chumba kimoja.

“Pamoja na hayo niliyoyasema pia nawashauri wamiliki wa hosteli kuweka mazingira ya vyoo vya hosteli vizuri na kutoa taarifa kwa wakati katika zahanati yetu mara wanafunzi wanaporipoti taarifa ya ugonjwa ili wanafunzi hao waweze kupatiwa matibabu haraka” Alisema dokta Neema.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Tarafa ya Hombolo afande Edwin Kitulo amewataka wamiliki hao kufanya usajili upya ili kutambua wanachuo na wasio wanachuo,kila mliki wa hosteli aweke mlinzi wa mchana na usiku ili kulinda usalama wa  wanachuo na mali zao na kuboresha miundombinu ya hosteli ikiwemo milango na madirisha ili kudhibiti wahalifu.

Akichangia mada katika kikao hicho Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Serikali za Mitaa bwana Najim alimuomba Mkuu wa polisi Tarafa ya Hombolo na kiongozi wa kampuni ya ulinzi chuoni hapo kuhakikisha usalama unakuwepo kuanzia chuoni mpaka mitaani kwa kuwa mara nyingi wanafunzi wanarudi kwenye hosteli za nje usiku na hivyo kuhatarisha usalama wao na pia aliwaomba wamiliki wa hosteli kuweka vyombo vya kuhifadhia taka ili kujilinda na magonjwa ya milipuko.

Kwa upande wao wao wamiliki wa hosteli hizo wameushukuru uongozi wa Chuo kwa kufanya nao kikao hicho na kuahidi kuyafanyia kazi yote yaliyojadiliwa ili kuwe na maelewano kati ya chuo na wao.

“Kwa niaba ya wamiliki wenzangu wa hosteli naupongeza uongozi wa chuo kwa kufanya kikao na sisi, hii ni nzuri sana ili tuwe na uelewa wa Pamoja lakini tunashauri uongozi wa chuo uwe unawasiliana na viongozi wetu kwa kila jambo ili iwe rahisi taarifa kutufikia kwa wakati kupitia viongozi wetu” Alisema Mzee Mbijima Mwenyekiti wa wamiliki wa hosteli.

Kikao hicho ni muendelezo wa uongozi wa Chuo cha Serikali za Mitaa kukutana na wadau mbalimbali wa chuo ili kuwekana sawa baadhi ya mambo kwa manufaa ya Chuo na jamii nzima inayokizunguka chuo hicho.


Announcements

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA OFISI YA RAIS -TAMISEMI KUJIUNGA NA CHUO May 27, 2022
  • FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023 May 18, 2022
  • KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2022/23 January 24, 2022
  • Approved Examination Results for Supplementary,Special and Carry Over for Semester I Academic Year 2021/2022 April 25, 2022
  • View All

Latest News

  • LGTI YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WAPYA

    April 12, 2022
  • LGTI yaingia mikataba ya Zaidi ya milioni 270

    March 10, 2022
  • Wadau wa Nyumba za kulala wanafunzi Hombolo wakutana na Uongozi wa Chuo

    December 31, 2021
  • LGTI yang’ara michezo ya SHIMIVUTA 2021

    December 19, 2021
  • View All

Video

Mafunzo ya Kituo cha Taarifa
More Videos

Quick Links

  • TCU Admission Almanac for 2021/2022 Admission Cycle
  • Student By-laws
  • OPRAS Forms
  • Institute's Almanac
  • Prospectus

Related Links

  • Tamisemi
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Dirisha la Hati ya Mshahara
  • Public Service Recruitment Secretariat

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Hombolo

    Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania

    Telephone: +255 26 296 1101

    Mobile: 736296110/712575754

    Email: info@lgti.ac.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Ghostwriter

    • Disclaimer
    • Privacy Policy

Copyright ©2021 Local Government Training Institute . All rights reserved.