• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff email |
Local Government Training Institute (LGTI)
Local Government Training Institute (LGTI)

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Local Government Training Institute (LGTI)

  • Home
  • About Us
    • Organization Structure
    • Vision and Mission
    • Objectives
    • Core Values
  • Administration
    • Board of Trustees
    • Workers Council
    • Office of the Rector
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
        • New menu item
      • Public Relations Unit
      • Information and Communication Unit
    • Planning, Finance and Administration
      • Department of Human Resource and Administration
      • Department of Accounting and Finance
      • Department of Policy and Planning
      • Department of Estate Management
      • Department of Health Services
  • Academics
    • Student Information System (SIS)
    • Mfumo wa Ujifunzaji Kielektroniki (MUKI)
      • Student Information System (SIS)
    • Department of Research, Short Course and Consultancy
    • Department of Human Resource Management
    • Department of Community Development
    • Department of Local Government Administration and Management
    • Department of Local Government Accounting and Finance
    • Department of Coordination and Quality Assurence
    • Department of Library Services
  • Admission
    • Online Application System (OAS)
    • Programs Offered
    • Entry Qualifications
    • Fee Structure
    • Prospectus
    • Joining Instructions
  • Students Welfare
    • Student Information System (SIS)
      • New menu item
    • Dean of Students
    • LOGISO
    • Hostels
    • Students By-laws
    • Campus Life
    • Almanac
  • Results
    • Appeal Form
  • Publications
    • Reports
    • Journals
    • Acts
  • Media Centre
    • Video Gallery
    • Photo Gallery
  • Library
    • Back Ground

Mamlaka za Serikali za Mitaa Zaagizwa Kutumia Chuo cha Serikali za Mitaa Kupata Mafunzo Elekezi

Posted on: December 18th, 2020


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhe. David Silinde, ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa zote nchini kukitumia Chuo cha Serikali za Mitaa kwa shughuli zote za mafunzo. Maagizo hayo ameyatoa leo Ijumaa terehe 18/12/2020 akiwa  ziarani chuoni Hombolo.  Mhe. Silinde amesisitiza kuwa Chuo cha Serikali za Mitaa ni taasisi ya mafunzo ya  Ofisi ya Rais TAMISEMI, hivyo, Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kote zikitumie Chuo chao kupata huduma za mafunzo.

“Naziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa zote nchini kuhakikisha kuwa huduma zote za mafunzo elekezi na mafunzo mengine yote kwa watumishi wa Halmashauri zinafanywa na Chuo cha Serikali za Mitaa kwa sababu kilianzishwa kwa lengo hilo na  kina wataalamu waliobobea, wenye uzoefu  na uelewa mkubwa wa masuala yanayoyohusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa.” alisisitiza.

Akizungumza na wajumbe wa menejimenti ya chuoni hapo alisema kuwa lengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI ni kuona Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaongeza tija katika utoaji wa huduma za jamii na usimamizi wa shughuli za maendeleo ya wananchi na hilo litafanikiwa iwapo viongozi, watumishi, na wananchi watawajibika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia shughuli zao.

“Inashangaza kuona Halmashauri zinatafuta watoa mafunzo ambao hawana uelewa mpana kuhusu namna Serikali za Mitaa zinavyofanya kazi na  matokeo yake  watumishi wake wanaendelea kufanya kazi kwa mazoea tu, pamoja na kwamba walipata mafunzo. Sasa ni vyema mamlaka hizo zikatambua kuwa kufanya hivyo ni makosa na kunaighalimu Serikali.” alisema Mhe. Silinde.

Akitoa ripoti ya mafunzo ya muda mfupi, Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Dr. Mpamila Madale, amesema kuwa Chuo cha Serikali za Mitaa kimejipanga vyema kutoa mafunzo elekezi kwa waheshimiwa madiwani wa Halmshauri zote nchini na tayari kimeshaanza kutoa mafunzo elekezi kwa waheshimiwa madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu  wa mwezi Oktoba,2020.  Mpaka sasa madiwani wa Halmashauri kumi nchini wameshapata mafunzo hayo.

Ziara ya Mhe. Naibu Waziri ilihusisha pia kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa na nyumba za watumishi ambazo zimejengwa kwa kutumia ‘Force Account’ kwa mapato ya ndani, ambapo aliweza kujionea majengo matatu ya kumbi za mihadhara, huku mawili kati ya hayo yakiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 504 kila moja na jingine lenye kumbi mbili zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 250 kila moja. Aidha mhe. Naibu Waziri aliweza kuona nyumba ya watumishi iliyojengwa  na Chuo yenye uwezo wa kukaliwa na familia mbili tofauti kwa wakati mmoja.

Mhe. Naibu Waziri alikipongeza Chuo kwa kuonesha mfano bora katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi huku kikibana matumizi bila kuathiri ubora.

“Haifai kutenga bajeti ya mradi wa maendeleo na kulazimisha kumaliza pesa yote hata kama mradi husika unatumia pesa pungufu ya kiasi kilichotengwa kwa ajili ya mradi.” aliongeza.

Akihitimisha mazungumzo yake na wajumbe wa menejimenti ya Chuo cha Serikali za Mitaa Mhe. Silinde alisisitiza kuwa kubana matumizi ni kumuunga mkono Mheshimwa Rais John Pombe Joseph Magufuli katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa miradi yote ya maendeleo nchini inaendana na thamani halisi ya pesa zinazotumika katika miradi hiyo.

Announcements

  • Control Numbers for Level 5 and 6 Tuition Fees- First Semester Installment November 19, 2020
  • Third Selection Certificate and Diploma November 25, 2020
  • Joining Instructions Form 2020 - 2021 October 30, 2020
  • Fee Payment Control Numbers for Certificate Students Academic Year 2020 2021 October 22, 2020
  • View All

Latest News

  • Matukio katika Picha

    December 28, 2020
  • Mamlaka za Serikali za Mitaa Zaagizwa Kutumia Chuo cha Serikali za Mitaa Kupata Mafunzo Elekezi

    December 18, 2020
  • Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo cha Serikali za Mitaa Wanolewa kuhusu Improved O&OD

    November 12, 2020
  • Training on Curriculum Implementation for Records Archives and Information Management and Procurement and Supply Management

    November 02, 2020
  • View All

Video

More Videos

Quick Links

  • Student By-laws
  • OPRAS Forms
  • Institute's Almanac
  • Prospectus

Related Links

  • Tamisemi
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
  • Dirisha la Hati ya Mshahara

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Hombolo

    Postal Address: P.O.Box 1125 Dodoma, Tanzania

    Telephone: +255 26 296 1101

    Mobile:

    Email: info@lgti.ac.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Ghostwriter

    • Disclaimer
    • Privacy Policy

Copyright ©2018 Local Government Training Institute . All rights reserved.